Mrithi wa Okwi : Athibitisha kuzungumza na Simba
Mganda Emmanuel Okwi safari yake ya Kuendelea kuichezea Simba
inaelekea Mwishoni na inaelezwa muda wowote ule kuanzia January Mwanzoni
Okwi atatangazwa kuwa mchezaji halali wa Kaizer Chief inayoshiriki ligi
kuu ya Afrika Kusini.
Inaelezwa kuwa kila kitu kiko vizuri kati ya Okwi na Kaizer Chief na
kati ya Kaizer Chief na Simba lakini bado viongozi wa Simba wamekuwa
wazito kulizungumzia suala hili la Okwi kuondoka January.
Mtandao maarufu zaidi wa michezo nchini Uganda Kawowo Sports
umethibitisha baadhi ya taarifa za Okwi kuwa amekubaliana na vipengele
vya mkataba wake na Kaizer Chief.
Wakati hayo yakiendelea msomaji wa Kwataunit.co.ke inaelezwa kuwa
Simba washaanza kumtafuta mrithi wa Emmanuel Okwi hasa wakati huu ambao
Simba inashiriki Hatua ya makundi klabu Bingwa barani Afrika.
Baada ya mchezo kati ya Simba na Nkana RED Devils ya Zambia ianelezwa
Simba walifanya mazungumzo na mchezaji na nahodha wa Nkana Fc Walter
Bwalya.
Alipotafutwa Walter Bwalya kuelezea kuhusiana na taarifa hizo
alifunguka na kusema kuwa ni kweli Simba walifanya mazungumzo na Waajili
wake Nkana Fc kuhusu usajili. ” ni kweli Simba baada ya mechi walifanya mazungumzo na
waajili wangu kwa ajili ya mimi kujiunga na wao. Mengine mtayajua muda
ukifika ”
No comments:
Post a Comment