Aliyekuwa kocha wa klabu ya Manchester United mwenye mafanikio
makubwa, Sir Alex Ferguson hii leo anatarajiwa kuwepo kwenye viunga vya
Carrington kumpa ushirikiano meneja wa sasa Ole Gunnar Solskjaer ambaye
ndiye aliyemualika.
Ferguson
atakuwa na furaha kubwa atakapomuona Solskjaer pamoja na benchi lake la
ufundi kwenye viwanja hivyo vya mazoezi vya Carrington wakati United
ikijiandaa kuwakabili Bournemouth siku ya Jumapili kwenye uwanjawa Old
Trafford.
Inaaminika kuwa Sir Alex Ferguson ndiye aliyempendekeza
kocha Solskjaer kuja kuifundisha United hadi mwisho wa msimu akitokea
Molde huku akiwa sambamba na Mike Phelan.
Straika huyo wa zamani wa United amejifunza vingi kutoka kwa Ferguson wakati alipokuwa akiitumikia timu hiyo.
Marakadhaa
amekuwa wazi juu ya matamanio yake ya kurudisha soka la kushambulia
zaidi ikiwa ni pamoja na tamaduni za United pamoja na kukuza vipaji vya
vijana wadogo kutoka kwenye academy.
‘’Nilikuwa na mwalimu mzuri,
siku zote alikuwa bora kwa hiyo utawala wangu utakwenda sambamba na vile
nilivyojifunza kutoka kwake,’’ amesema Ole Gunnar Solskjaer.
Hii
si mara ya kwanza kwa kocha huyo kualikwa itakumbukwa hata, Jose
Mourinho aliwahi kufanya hivyo lakini Ferguson alishindwa kuhudhuria
kwenye viwanja hivyo vya Carrington kufuatia kufanyiwa upasuaji wa
ubongo.
No comments:
Post a Comment