Kocha wa Arsenal, Unai Emery amewaomba radhi mashabiki wa klabu ya
Brighton baada yakumpiga na chupa mmoja kati ya mashabiki wa timu hiyo
kwenye mchezo uliyomalizika kwa sare ya bao 1- 1. Muhispania
huyo aliipiga teke chupa ya maji na kumrukia mmoja wa mashabiki
waliyokuwa uwanjani hapo na kuomba radhi muda huo huo kwa kitendo hicho. Kwenye tukio hilo, Emery alionekana kwenda upande wa mashabiki na kumuomba radhi yule aliyoguswa na chupa hiyo. Baada
ya mchezo kocha huyo alielezea kile kilichotokea ‘’Niliwaambia
samahani, kwasababu nilipiga teke chupa iliyompata shabiki mmoja baada
ya kuvunjika moyo kwa matokeo yalivyokuwa yanaonekana dakika za
mwisho,’’ amesema Emery. Unai Emery ameongeza ‘’Haikuwa nzito, lakini ilimgusa mmoja kati ya mashabiki na niliwaomba radhi.’’ Mesut Ozil aliingia kwenye kipindi cha
pili lakini ameshindwa kuisaidia Arsenal kupata matokeo.
No comments:
Post a Comment