Monday, 14 January 2019

Manchester City 3-0 Wolves: Gabriel Jesus afungia City mawili na kupunguza uongozi wa Liverpool

Download ,Install App bora ya Habari na michezo

 

Gabriel Jesus alifunga mabao mawili na kuwawezesha Manchester City kuwalaza Wolves mabao 3-0 na kupunguza uongozi wa Liverpool kileleni hadi alama nne.
City hawakuweza kurejelea ufungaji wa mabao mengi ambao walikuwa wameandikisha dhidi ya Rotherham (7-0) na Burton (9-0), ambapo kwa jumla walikuwa wamefunga mabao 16.
Lakini si wengi walikuwa na shaka kwamba wangeibuka washindi, ingawa kwa mabao machache. Hata hivyo, wapo waliotarajia Wolves watoe ushindani mkali ikizingatiwa kwamba wamekuwa mwiba kwa klabu kubwa.
Jesus alianza ufungaji wa mabao dakika ya 10 pale Leroy Sane alipoifikia pasi kutoka kwa Aymeric Laporte na akamwandalia Mbrazil huyo mpira safi na kumuwezesha kufunga.

Kibarua ambacho tayari kilikuwa kigumu kwa Wolves kiligeuka na kuwa kigumu hata zaidi pale Willy Boly alipofukuzwa uwanjani dakika ya 19 kwa kumchezea visivyo Bernardo Silva. Alionyeshwa kadi nyekundu moja kwa moja.
City mwanzoni walionekana kutotumia wingi wa wachezaji uwanjani kujifaidi na walipata wasiwasi pale Jonny alipokaribia sana kufunga kutoka kwa pasi ya Diogo Jota, katika shambulio nadra sana la wageni.
Hilo liliwazindua City na dakika chache baadaye, wakaongeza uongozi wao kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 39.
Ryan Bennett alimwangusha Raheem Sterling eneo la habari na Jesus akafunga mkwaju waliozawadiwa.

Swali kuu baada ya mapumziko lilikuwa City wangefunga mabao mangapi, ikizingatiwa kwamba vijana hao wa Pep Guardiola walikuwa wamefunga mabao matano kipindi cha pili dhidi ya Burton katika Kombe la Carabao na manne dhidi ya Rotherham katika Kombe la FA.
Hata hivyo, dhidi ya Wolverhampton Wanderers, walipata bao moja pekee.
Nguvu mpya Kevin de Bruyne alitoa krosi na Conor Coady akajifunga na kukamilisha ushindi wa City dakika ya 78.


Download ,Install App bora ya Habari na michezo

City washindwa kufikia rekodi

City walikuwa bado wanatafuta magoli zaidi, lakini walimaliza mechi wakiwa bado wanatafuta bao moja kutimiza mabao 100 katika mashindano yote msimu huu.
Hii ina maana kwamba walipoteza fursa ya kufikia rekodi walioweka wenyewe msimu wa 2013-14 kwa kuwa klabu ya kwanza kabisa kufikia mabao hayo enzi ya Ligi ya Premia kwa kasi zaidi.

Kwa sasa, ndio klabu iliyofunga mabao mengi zaidi Ligi ya Premia - 59.
Leo Jumanne ni mwezi mmoja tangu City walipokuwa kileleni kwenye jedwali, na Liverpool sasa wamewazidi City kwa kuwa klabu ambayo imesalia kileleni muda mrefu zaidi msimu huu. Liverpool wameongoza siku 75 sasa, City wakaongoza siku 74.
Wolves walazimishwa 'kujiepushia aibu'
City walipotez alama za kwanza msimu huu walipotoka sare ya 1-1 uwanjani Molineux Agosti na Nuno Espirito Santo na vijana wake walithibitisha kwamba matokeo hayo hayakuwa ya kubahatisha kwa kuwakaba koo Chelsea, Manchester United, Tottenham na Liverpool.


Lakini Jumatatu, walishindwa kuwazidi ujanja City, hasa baada ya Boly kufukuzwa uwanjani.
Walishindwa pia kuupata mpira.
Walikamilisha pasi 271 pekee wakilinganishwa na City waliokamilisha pasi 870. Pasi nyingi za Wolves zilikuwa katika eneo lao.
Katika mechi yote, ilikuwa wazi kwamba walikuwa wanacheza kujiepushia kipigo kikubwa.

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola aliambia BBC Sport baada ya mechi kwamba: "Wanajilinda sana kwenye ngome yao hata wakiwa wachezaji 10 na kwa hivyo si rahisi hata ukiwana mchezaji mmoja zaidi.
Kevin [de Bruyne] aliingia uwanjani [dakika ya 62] na kutoa krosi mara 10.
"Hiyo ndiyo njia tunayolazimika kucheza [katika hali kama hiyo]. Kama utacheza mpira wa pasi, pasi, pasi basi itakuwa vigumu.

Nuno Espirito Santo alisema kadi nyekundu aliyolishwa Boly iliwaumbua: "Sio kwamba tu kadi hiyo nyekundu ilibadilisha mchezo, lakini jinsi tulivyofungwa kutokana na pasi ya mbali. Kadi nyekundu inafanya mambo kuwa magumu zaidi.
"Unajua ni vigumu kuwazuia lakini ni lazima ujaribu kukwepa hali nyingine na hiyo pasi ya hatua 30 ni lazima tujaribu kujiboresha [hatukufaa kufungwa]. Lakini hauwezi kupanga mchezo ukiwa na upungufu wa mchezaji mmoja.
"Ni lazima uhakikishe unasalia kwenye mechi na kutia bidii hadi mwisho, na vijana wangu walifanya hivyo na kwa hivyo sasa tunatazama siku zinazofuata na kibarua kijacho ni nyumbani sasa."
Nini kinafuata?
Wolves watakuwa nyumbani dhidi ya Leicester Jumamosi nao Manchester City wasafiri ugenini kukutana na Huddersfield Town Jumapili, mechi ambayo itakuwa ya kwanza kwa Huddersfield tangu meneja wao David Wagner kuondoka.

Download ,Install App bora ya Habari na michezo


No comments:

Post a Comment