Thursday, 31 January 2019

Matokeo Yanga vs Biashara United leo 31 January 2019

Download ,Install App bora ya michezo

Matokeo Yanga vs Biashara United leo 31 January 2019
Matokeo mechi ya Kombe la Shirikisho Azam Sports Federation Cup kati ya Yanga dhidi ya Biashara United
Mechi Imeanza
Yanga 0 – 0 Biashara United
Dakika ya kwanza Biashara United wanapata penati baada ya Dante Kumuweka chini mchezaji wa Biashara United
Dante anapewa kadi ya njano
Goaaaaaaaal Waziri Junior anaipatia Biashara United bao la Kuongoza
Yanga 0 – 1 Biashara United
Dakika ya 7 Yanga nao wanapata penati baada ya Ibrahim Ajibu kuweka chini ndani ya 18
Goaaaaaaal Dakika ya 8 Amis Tambwe anafunga penati na kuisawazishia Yanga
Yanga 1 – 1 Biashara United
Dakika 15
Yanga 1 – 1 Biashara United
Dakika ya 21 Biashara United wanakosa goli la wazi
Dakika ya 24 Gadiel Michael anajaribu kupiga Shuti langoni mwa Biashara lakini shuti lake linaishia mikononi mwa Kipa
Dakika ya 31 Yanga wanapata kona
Dakika ya 32 Yanga wanapata kona Nyingine
Goaaaaaaaal dakika ya 40 Innocent Edwin anaitanguliza Biashara United kwa bao safi
Yanga 1 – 2 Biashara United

HALF TIME

Yanga 1 – 2 Biashara United
KIPINDI CHA PILI
Kipindi cha Pili kimeanza
Yanga 1 – 2 Biashara United
Dakika ya 46 Mrisho Ngassaa anapewa kadi ya njano baada ya kumchezea madhambi Derrick Mussa
Dakika ya 49 Yanga wanapata Kona wanashindwa kuitumia vyema
Dakika ya 50 Mrisho Ngassa anawekewa pasi nzuri an Ajibu lakini anapiga shuti linalopaa juu ya lango
Dakika ya 59 Mwamuzi Martin Sanya anampa kadi ya Njano Paul Godfrey
Dakika ya 60 Thaban Kamusoko anaingia kuchukua nafasi ya Pius Buswita
Dakika ya 60 Mangalo anapewa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Ngassa
Dakika ya 61 Yanga wanakosa nafasi ya wazi mpira ukabaki kuwa unazengea langoni mwa Biashara kabla ya kipa Nurdin Barola kuudaka
Dakika ya 64 Yanga wanakosa tena bao hapa kichwa cha Makambo kinaokolewa na beki kwenye chaki
Yanga wanapata kona mbili mfululizo
Wanapata Kona nyingine dakika ya 69 lakini kabla ya kuwafikia wachezaji wa Yanga wanamchezea faulo kipa Nurdin Barola
Goaaaaaal Heritier Makambo anaisawazishia Yanga, Dakika ya 73
Yanga 2 – 2 Biashara United
Wakati huo huohuo Tambwe ametoka na Matheo Anthony anaingia kuchukua nafasi yake.
Biashara United wanafanya mabadiliko ya kumtoa Kipa Barola anaingia kipa Mwingine Hassan Robert
Baada ya kipa kutolewa anaonekana kumlaumu kocha wake kwanini amemtoa



Zimeongezwa Dakika 5 kumaliza mechi
FULL TIME
Yanga 2 – 2 Biashara United
PENATI ZINAFATA
Yanga 5 – 4 Biashara United
Yanga wanafuzu hatua inayofuata

Download ,Install App bora ya michezo

 

No comments:

Post a Comment