Saturday, 12 January 2019

Muache Okwi aitwe Okwi aonyesha balaa

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa timu ya Simba raia wa Uganda, Emmanuel Okwi anafanikiwa kuonyesha thamani yake ya umataifa kwa kufunga bao maridadi kabisa dakika ya 45 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya JS Saoura Uwanja wa Taifa.

Okwi alifanikiwa kutumia uwezo wake wa mguu wa kushoto kumalizia pasi ya Clyetous Chama ambaye alipiga pasi mpenyezo iliyomkuta Okwi akawaminya mabeki waarabu na kumalizia kwa shuti kali.

Kwa sasa mpira ni kipindi cha pili huku kila timu ikiwa imepania kupata matokeo, katika harakati za kipindi cha kwanza nahodha John Bocco alipata majeraha akatoka nafasi yake ikachukuliwa na Meddie Kagere.

Download ,Install App bora ya michezo

No comments:

Post a Comment