Neymar JrKwa mujibu wa gazeti la EL Mundo Deportivo la Hispania, limeeleza kuwa baba yake na Neymar ameshatuma maombi ya mtoto wake kurudi kwenye klabu hiyo.
Gazeti
hilo limeeleza kuwa, Barcelona wamekubali ombi lake, lakini kwa
masharti ya kumtaka afute kesi ya madai ya Euro Milioni 30, ambayo
anaidai klabu hiyo tangu alivyovunja mkataba wake mwaka 2017.
Imeelezwa kuwa Neymar Jr kwa sasa hana furaha na timu yake ya PSG.
Wakati
hayo yakijiri, mshambuliaji wa mabingwa hao wa Hispania, Phillipe
Coutinho yupo mbioni kuuzwa na klabu hiyo ili kupunguza gharama za
usajili wa Neymar.
No comments:
Post a Comment