Polisi mjini Las Vegas wametoa waranti ya kuchunguzwa kwa chembe
chembe za vinasaba au DNA ya Cristiano Ronaldo kama sehemu ya uchunguzi
wa madai ya ubakaji dhidi ya nyota huyo wa kimataifa wa Ureno
anayechezea klabu ya Juventus.
Kwa mujibu wa BBC, Wakili, Peter S. Christiansen, ameiambia BBC Michezo kuwa ombi hilo ”ni la kawaida”.
Jarida la Wall Street limeripoti kuwa waranti hiyo imewasilishwa hivi karibuni katika mfumo wa mahakama ya Italia.
Ronaldo amekanusha kwamba alimshambulia mwanadada Kathryn Mayorga katika mgahawa mmoja mjini Las Vegas hotel mwaka 2009.
”Bwana
Ronaldo amekua akishikilia usemi kuwa yale yaliyotokea Las Vegas mwaka
2009 ni mambo ya watu wawili waliyokubaliana, kwa hiyo bila shaka chembe
chembe za DNA zitapatikana, kwa hiyo sioni haja ya polisi kutoa ombi
hilo kama sehemu ya uchunguzi wao,”ilisema taarifa ya Christiansen.
Gazeti
la Der Spiegel la Ujerumani ambalo lilikuwa la kwanza kuangazia taarifa
hiyo mwezi Oktoba, lilisema kuwa Bi Mayorga aliandikisha ripoti katika
kituo cha polisi cha Las Vegas muda mfupi baada ya kufanyika kwa tukio
linalodaiwa.
Der
Spiegel lilisema kuwa mwaka 2010, Mayogra aliafikiana na Ronaldo
kutatua suala hilo nje ya mahakama ambapo alilipwa dola 375,000
ilisizungumza hadharani madai hayo.
Mawakili wake sasa wanahoji kuwa makubaliano hayo hayakuwa rasmi.
Wakili
wa Ronaldo amewahi kusema kuwa mteja wake hakukataakutia saini
makubaliano hayo “sababu zilizomfanya kufikia uamuzi huo zimepotoshwa”.
Aliongeza: ”Hatua hiyo haimaanisha amekiri kuwa na makosa.”
Bi
Mayorga alipata ujasiri wa kuzungumzia masaibu yake kutokana na
kampeini ya #MeToo movement, ambayo imekuwa ikiendeshwa mtandaoni.
Wakili wake amesema kuwa mteja atamfungulia mashtaka Ronaldo nchini Marekani.
Ronaldo alihamia Juventus kutoka Real Madrid mwezi Julai kwa kima cha euro 99.2.
Ameshinda tuzo ya Ballon d’Or – ambayo hupewa mchezaji bora wa soka duniani – mwaka 2008, 2013, 2014, 2016 and 2017.
Nyota
huyo wa kimataifa wa Ureno aliwahi kupinga madai dhidi yake kama
“taarifa ghushi” na baadae mwezi Oktoba akatoa taarifa kupitia mtandao
wake wa Twitter ambapo alipinga “vikali” suala hilo.
Wakili
wake anadai kuwa stakabadhi za uchunguzi zilizotumiwa na gazeti la Der
Spiegel ”ni za kubuniwa” lakini gazeti hilo linasema “halina sababu” ya
kutilia shaka uhalisia wake.
No comments:
Post a Comment