Download ,Install App bora ya Habari na michezo
Taarifa ya Coastal Union kuhusu msiba wa baba yake Ali KibaBaada ya Taarifa za Msiba wa baba yake Ali Kiba ambaye ni mchezaji aliyesajiliwa na Coastal Union msimu huu hii ndiyo Taarifa waliyoiandika Coastal Union kwenye kurasa zao za mitandao ya Kijamii.
TANZIA
Uongozi wa Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ unaungana na familia ya mchezaji wake Ally Saleh Kiba, kutokana na msiba walioupata kwa kuondokewa na baba yake mzazi. Mzee Saleh.
Mauti yamemkuta mzee wetu leo asubuhi jijini Dar es Salaam na maziko yatafanyika leo hapahapa Dar es Salaam.
Wanachama na wapenzi wa Coastal Union, unatambua hali ngumu anayopitia mchezaji wetu, nasi tunamfariji na kusisitiza msiba huu ni wetu sote.
Mshituko wa kumpoteza mzazi hauvumiliki, lakini Mungu ana makusudi yake kwa kila kinachotokea juu ya mgongo wa ardhi.
Pole ndugu yetu Ally Kiba na pole kwa wanafamilia.
Sote ni waja wa Mwenyezi Mungu na Kwake tutarejea.
HAFIDH KIDO
MSEMAJI COASTAL
17/01/2019
No comments:
Post a Comment