Barcelona imesema iko tayari kupokea ofa ya kumnunua kiungo wao wa kati
Philippe Coutinho, 26. Manchester United imeonyesha nia ya kumsaini
mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool katika wakati wa msimu wa joto.
(Calciomercato, via Star) Barcelona pia wameweka dau la pili la kumnunua
Willian ambaye ni winga wa Chelsea na Brazil, baada ya ofa yao ya
kwanza ya kumnunua kiungo huyo wa miaka 30 kugonga mwamba siku ya
alhamisi. (Standard)
Chelsea imekubali kuwanunua kwa masharti viungo wa kati Nicolo
Barella, 21, kutoka klabu ya Cagliari na Leandro Paredes, 24, wa klabu
ya Zenit St Petersburg(Telegraph)
Meneja wa AC Milan Gennaro
Gattuso amesema kuwa klabu hiyo inaendelea kuzungumza na wawakilishi wa
mshambuliaji Gonzalo Higuain licha ya tetesi kuwa mshambuliaji huyo
huenda akahamia Chelsea. (Express)
Kumsaini kwa mkopo Higuain hadi mwisho wa msimu huu ndio mpango wake wakati huu wa uhamisho wa wachezaji. (Sun) Baba
yake Neymar ambaye ni nyota wa kamtaifa wa Brazil na Paris St-Germain
amepinga uvumi kuwa nyota huyo wa miaka 26 anataka kurejea katika klabu
yake ya zamani Barcelona. (Express)
Liverpool na Fulham wote
wanataka kumsaini mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na Israel Moanes
Dabour, 26. (Estadio Deportivo – in Spanish)
Meneja wa Everton
Marco Silva amesema hana hofu hata ikiwa klabu yake haitaongeza mchezaji
yeyote wakati huu ambapo dirisha la uhamisho wa wachezaji liko wazi.
Marcos hata hivyo ameongeza kuwa angelipendelea kuwasaini wachezaji “wawili watatu” wapya . (Liverpool Echo)
West Ham wanatafakari uwezekano wa kumhamishia Newcastle kiungo wake wa kati Jonjo Shelvey. (Mail)
Leeds wanajiandaa kumsaini kipa wa Real Madrid Kiko Casilla.
Kipa huyo wa miaka 3anatarajiwa kusafiri England wiki ijayo. (Yorkshire Evening Post)
Vilabu
kadhaa vinavyoshiriki ligi kuu ya Italia Serie A vimeonyesha azma ya
kumnunua kiungo wa kati wa Aston Villa na Congo Aaron Tshibola, 24.
Tshibola amekuwa akicheza kwa mkopo katika uga wa Kilmarnock msimu huu. (Birmingham Mail)
Juventus
wana mpango wa kumsaini tena Paul Pogba, 25, Manchester United endapo
winga wa Brazil Douglas Costa, 28, atahamia Old Trafford kama sehemu ya
mpango huo. (Tuttosport, via Calciomercato) Juventus
pia wako tayari kumuachilia beki wa kati wa Morocco Medhi Benatia, 31,
kuenda Arsenal katika hatua ambayo itamwezesha Aaron Ramsey, 28, kuhamia
upande wowowte. (Gazzetta dello Sport, via Metro)
Barcelona wanatafakari uwezekano wa kumchukua mshambulaji wa Chelsea na Uhispania Alvaro Morata, 26 kwa mkopo.
Morata huenda akanunuliwa na Sevilla na Atletico Madrid. (Sport – in Spanish)
Nahodha wa Arsenal Laurent Koscielny, 33, amekataa ombi la Monaco la kutaka ajiunge nao. (Le10 Sport, via Mirror) Monaco wamezungumza na Chelsea kuhusu mpango wao wa kumnunua mshambuliaji wa Ubelgiji Michy Batshuayi, 25.
Agenti wake wameenda Ufaransa kujadili uwezekano huo. (Goal)
Everton wameonesha nia ya kumsajili mlinzi wa Southampton na Portugal Cedric Soares, 27. (Sun, via Star)
Winga
wa Hull City Jarrod Brown wa huenda akasainiwa na Leicester City huku
Tottenham na Everton wakimfuatilia kiungo huyo wa miaka 22. (Sun)
Hull wanakaribia kumaliza mchakato wa kumsaini kwa mkopo mlinzi wa Cardiff City Matthew Connolly, 31. (Hull Daily Mail)
No comments:
Post a Comment