Saturday, 26 January 2019

Timu 10 Kazini ligi ya wanawake Tanzania

Download ,Install App bora ya michezo


Leo Jumapili, Ligi ya wanawake Tanzania maarufu kama Serengeti Lite Women's Premier League inaendelea kwa timu 10 kushuka Uwanjani kumenyana kutafuta pointi tatu.

Wababe JKT Queens leo watamenyana na Marsh Queens Uwanja wa Maj.Gen.Isahmuyho.

Alliance Girls watamenyana na Baobab Queens Uwanja wa Nyamagana.

Sisterz FC watamenyana na Tanzanite SC Uwanja wa Lake Tanganyika.

Mlandizi Queens atakuwa mzigoni leo dhidi ya EverGreen Queens Uwanja wa Mlandizi.

Simba Queens atakuwa kazini akimenyana na Panama FC Uwanja wa Karume.

Mechi zote zitaanza jioni ya saa 10:00 kwa saa za Afrika mashariki.

Download ,Install App bora ya michezo

No comments:

Post a Comment