Wednesday, 6 February 2019

Matokeo Singida United vs Yanga 6 February 2019

Matokeo Singida United vs Yanga 6 February 2019
Matokeo Kati ya Singida United dhidi ya Yanga leo 6 February 2019 kutoka uwanja wa Namfua mkoani Singida
Kuanzia saa kumi kamili Tutakupa Matokeo Live
Mechi Imeanza
Singida United 0 – 0 Yanga
Dakika ya 3 Mathew Michael wa Singida United yupo chini baada ya Kuumia, Madaktari wanaingia Kumtibu
Pambano Linaendelea
Dakika ya 4 Singida United wanapata Kona lakini wanashindwa kuitumia kupata bao
Dakika ya 5
Singida United 0 – 0 Yanga
Dakika ya 8 Yanga wanakosa bao la wazi baada ya Kaseke kuukosa mpira uliopigwa na makambo, Kipa Said Lubawa anaokoa kabla ya Kaseke hajaugusa
Dakika ya 10 Matheo anajaribu shuti nje ya 18 inakuwa nyepesi kwa kipa Said Lubawa wa Singida United
Dakika ya 15
Singida United 0 – 0 Yanga
Dakika ya 16 Yondani almanusra achomeshe lakini pasi aliyompa Kyombo inatoka nje kidogo ya Lango
Dakika ya 18 Makambo almanusra aiandikie Yanga bao lakini mpira anaoupiga unaokolewa na Kipa Said Lubawa na kuwa Kona
Dakika 20
Singida United 0 – 0 Yanga
Dakika ya 22 Paul Godfrey anaingia kwa kasi na kuwalamba vyenga walinzi wa Singida lakini shuti lake linapita nje kidogo ya Lango
Dakika ya 24 Boniface MAGANGA anapewa kadi ya njano kwa kumzuia Kabwili kupiga mpira
Dakika 30
Singida United 0 – 0 Yanga
Dakika ya 34 Yanga wanapata Kona ni ya tatu kwa Yanga katika mchezo wa leo
Dakika ya 36 Habib Haji Kyombo anajaribu shuti kali linaenda nje ya lango la Yanga
Dakika ya 37 Yanga wanapata Kona
Dakika 40
Singida United 0 – 0 Yanga
Dakika ya 45 Ramadhan Kabwili anafanya save nzuri ambayo kama si yeye Yanga wangekuwa wametanguliwa na Singida kwa bao 1

HALF TIME

Singida United 0 – 0 Yanga

KIPINDI CHA PILI

Kipindi cha Pili kimeanza
Singida United 0 – 0 Yanga
Dakika ya 46 Yanga wanapata free Kick baada ya Fei Toto kuwekwa chini nje kidogo ya
Dakika ya 48 Yanga wanakosa bao jingine la wazi baada ya Free Kick, Kipa aliokoa kisha mpira ukawahiwa na Matheo akapiga krosi pasi kipa akaokoa tena mpira ukamkuta Feisal Salum ambaye anapiga shuti linaloenda nje ya Lango
Dakika ya 50
Singida United 0 – 0 Yanga
Dakika ya 55 Feisal Salum anapewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi mchezaji wa Singida United
Dakika ya 59 anatoka Matheo Anthony na Yondani wanaingia Andrew Vincent na Pius Buswita
Dakika ya 61 Gustafa Simon anajaribu shuti langoni mwa Singida linapaa juu ya Lango
Dakika ya 62 Yanga wanapata kona
Dakika ya 64 Mwashiuya anaingia kuchukua nafasi ya Athanas Mdamu
Dakika ya 67 Kennedy Juma Anapewa kadi ya njano
FDakika ya 67 eisal Salum anatoka anaingia Ibrahim Ajibu
Dakika 75
Singida United 0 – 0 Yanga
Dakika ya 77 Ajibu anamtengea pasi Nzuri Makambo lakini Makambo anashindwa kuwajaza Singida

Dakika ya 80
Singida United 0 – 0 Yanga
Yanga wanapata Free Kick nje kidogo ya Lango
Dakika ya 90 Heritier Makambo anaonyeshwa kadi ya njano

FULL TIME

Singida United 0 – 0 Yanga

No comments:

Post a Comment