Mwili ulioopolewa kutoka kwenye mabaki ya ndege iliyoanguka ni wa
mchezaji soka wa timu ya Cardiff City, Emiliano Sala Polisi ya Dorset
imesema.
Sala, mwenye umri wa miaka 28, alikuwa akisafiri kwenda Cardiff
ikatika ndege ambayo rubani wake alikuwa ni David Ibbotson, iliyopotea
mnamo Januri 12.
Mwili wake ulipatikana Jumatano baada ya kugunduliwa kwa mabaki ya ndege hiyo Jumapili asubuhi.
Polisi ya Dorset imethibitisha utambulisho wake Alhamisi usiku.
Katika taarifa yake, kikosi hicho kimesema: “mwili ulioletwa katika
bandari ya leo Alhamisi Februari 7 2019, umetambuliwa rasmi kuwa wa
mchezaji soka Emiliano Sala.
“Familia ya Sala na rubani David Ibbotson wamearifiwa kuhusu taarifa
hii na wataendelea kupewa usaidizi na maafisa wa kitengo maalum.”
Kikosi cha uchunguzi wa ajali ya ndege awali kilieleza kwamba
wakandarasi maalum wamejiunga katika operesheni hiyo, katika ‘hali yenye
changamoto nyingi’.
Imefanyika ‘kwa heshima kubwa iwezekanavyo’ na familia za wote wawili ziliarifiwa kadri shughuli zilivyokuwa zikiendelea.
Mabaki ya ndege hiyo, iliyopotea wiki mbili zilizopita, yalipatikana kutoka huko Guernsey.
Ndege hiyo chapa Piper Malibu N264DB ilikuwa ikielekea kutoka
Ufaransa kwenda Cardiff, baada ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka
28 raia wa Argentina kurudi kwa safari ya haraka katika klabu yake ya
zamani Nantes siku mbili baada ya kutangazwa kuidhinishwa kwa mkataba
wake wa thamani ya £15m kwenda Cardiff . Image captionMashabiki wa Cardiff wakiwaweka mashada ya maua wakimuombea kheri Emiliano Sala
Ibbotson, mwenye umri wa miaka 59, kutoka Crowle, Lincolnshire
kaskazini, alikuwa kwenye mawasiliano na waongoza ndege ardhini ndege
hiyo ilipokatiza mawasiliano na kupotea kwenye rada mnamo Januari 21.
Shughuli rasmi ya kuisaka ndege hiyo ilisitishwa Januari 24 baada ya
mamlaka kudai uwezekano wa kupatikana hai wawili hao ulikuwa “mdogo
mno”.
Hata hivyo, mabaki ya ndege hiyo yalipatikana chini ya bahari baada
ya wasamaria wema kuchangisha fedha zilizowezesha operesheni ya binafsi
iliyoongozwa na mwanasayansi ya bahari David Mearns. Image captionMashabiki wa Nantes pia wamekuwa wakimkumbuka Sala
Juhudi za kuinyanyua ndege hiyo toka chini ya bahari zimeshindikana kwa sasa kutokana na hali mbaya ya hewa.
No comments:
Post a Comment