Tangawizi
Ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika kutokana na mmoja wa wanadoa hoa
kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa bila kujua kuwa vipo vyakula
tunavyokula vinavyoweza kuchangia chemistry ya miili yetu kuhusiana na
suala la hamu ya kushiriki tendo la ndoa.Miongoni mwa vyakula hivyo ni
pamoja na :
KARANGA
Karanga huhusika moja kwa moja na kutunza mfumo wa mzunguko wa damu
kuwa na afya (vascular system).Pia mfumo wenye afya (mzunguko wa damu)
katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa
mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa zuri na kulifurahia.
Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic
na zinc ambayo ni muhimu sana katika uzalishaji wa mbegu za mwanaume.
TANGAWIZI
Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa
damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda
sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume.
Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama unga.
PILIPILI
Kama tunavyojua chakula ambacho kimeungwa na pilipili hufanya hata
mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho kutoka au
kamasi kutoka.
Kwenye pilipili kuna kitu kinaitwa capsaicin ambacho hufanya
pilipili iwe na hali ya ukali ambao huwezesha ubongo kutoa homoni ya
endorphins ambayo katika hali ya juu huleta mguso wa hisia za raha.
Pia pilipili husisimua mfumo wa ufahamu (nerves) wa ubongo na
katika kufanya hivyo huwezesha kuamsha haraka hisia za mapenzi na pia
usaidia mwili kuwa na hisia za haraka zaidi kwa kuguswa na kadhalika.
ASALI
Asali ina madini yanayoitwa boron, ambayo husaidia mwili kutumia
homoni ya estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo ya uzazi na
mapenzi kwa mwanamke.
Pia utafiti unaonesha kwamba asali huongeza nguvu, kitendo ambacho kitapelekea mwanamke kuwa na uwezo wa hamu ya tendo la ndoa.
MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI.
Mlo wenye matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi.
Kwanza matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na
unene (cholesterol), kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa
damu kwa kubana mishipa ya damu.
Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha balance ya uzito
kwani unene (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya katika kuzalisha
homoni za testoeterone na hatimaye jogoo kushindwa kuwika na kuwa na
tatizo la kukosa hamu ya tendo.
Na pia wanandoa wanapozidi kunenepeana ndipo na hali ya kufurahia, kutaka au kuwa na hamu ya tendo la ndoa huzidi kupungua.
NAFAKA
Nafaka zina nyuzinyuzi (fibre) na sukari ngumu (complex sugar) ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili.
Nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu.
Na pia nafaka huwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa tendo.
Kula nafaka kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula
nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri linalokuhakikishia afya
njema na mahusiano mazuri ya ndoa yako.
CHOCOLATE
Chocolate ina phenylethylamine, kemikali ambayo husababisha hisia
(feelings) za furaha wakati mwanamke au mwanaume anapofika kileleni
(orgasm)
OYSTERS
Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na haya madini ndiyo
huhusika zaidi na uzalishaji wa homoni ya testosterone kwa wanaume.
Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini ya zinc
huwa na matatizo ya nguvu za kiume na wakati huohuo kuwa na madini mengi
ya zinc mwilini huongeza kiwango cha shahawa.
SOYA
Pamoja na kuwa na kiwango kidogo sana cha fat na pia kuwa na
kiwango kizuri cha protein, soya zina phytoestrogens ambayo husaidia
sana wanawake ambao wamefikia menopause kutengeneza homoni estrogen ya
ziada.
Husaidia uke kuwa laini (wet, lubricated) hali inyomfanya mwanamke kufurahia tendo bila maumivu wakati wa tendo la ndoa.
No comments:
Post a Comment