Friday, 26 April 2019

Manara: Angaikeni na Mishahara siyo timu Bingwa




Manara: Angaikeni na Mishahara siyo timu Bingwa

Wakati jana kukiwa na taarifa kuwa Wachezaji wa Yanga waligoma kufanya mazoezi kwa madai ya kutaka kulipwa mishahara yao basi Haji Manara ambaye ni afisa habari wa Simba ameamua kupita nao na kuwatupia dongo Yanga,
Manara amepita na dongo hilo kutokana na washabiki wengi wa Yanga kukosoa maamuzi ya jana dhidi ya KMC wakiamini Simba alibebwa katika mchezo hu.
Manara kupitia Instagram yake ameandika.
Badala ya kuhangaika jinsi ya kuwalipa mishahara wachezaji wenu mnahangaika na team Bingwa inayowafunga kila siku!!
Bumbaaav,afungwe KMC kiherehere kiwakumbe Makwasukwasu!!
Kama nyie Wananchi wachangieni hao wachezaji!!

No comments:

Post a Comment