BEKI na nahodha wa Azam FC, Aggrey Morris amefichua hataacha
kumkumbuka John Bocco aliyeitumikia timu hiyo kwa mafanikio ya hali ya
juu kabla ya kuhamia Simba kutokana na mchango wake ambao kwa sasa
wanaukosa.
Alisema Bocco alikuwa na mchango mkubwa ndani ya Azam na kudai mchango wake ni ngumu kusahaulika, hukua kidai ni na kuigwa na chipukizi ambao wanakuja nyuma yake.
“Ukizungumzia Bocco unazungumzia mchezaji mkubwa na mwenye mafanikio makubwa katika soka la Tanzania, ameondoka Azam FC akiwa ameacha mataji ya ligi, shirikisho, Kagame na Mapinduzi. “Bado moto wake hajazima katika timu yake ya Simba msimu uliopita alifunga mabao 14, pia anaendelea kufanya vizuri timu hiyo inaposhiriki ligi ya Mabingwa Afrika, nakumbuka namna ambavyo alikuwa muhimu katika safu ya mbele,” alisema.
Alisema Bocco ni kati ya washambuliaji wanaowapa wakati mgumu mabeki kutumia akili kubwa kumkaba anapokuwa ndani ya 18.
“Namna nilivyo mimi namheshimu straika yoyote ule ninapokuwa kwenye na majukumu uwanjani, kazi yangu ni kuzuia mashambulizi, ndio maana nimesema Bocco ni straika hatari anapokuwa eneo lake la kujidai,”alisema.
Mbali na kuzumnguzia Bocco pia ameeleza wanahitaji kuongeza umakini ili kuweza kukata tiketi katika Kombe la FA na ligi kuu Bara ya kushiriki michuano ya kimataifa.

No comments:
Post a Comment