Monday, 31 December 2018

Ilipofikia ishu ya Okwi kutua Kaizer Chief Simba wafunguka haya

Ilipofikia ishu ya Okwi kutua Kaizer Chief Simba wafunguka haya
Wiki kadhaa zilizopita vyombo vingi vya habari ndani na nje ya Nchi anakotoka Mganda Emmanuel Okwi viliripoti juu ya klabu ya Kaizer Chief kumhitaji straika huyo kutoka Simba.

Ratiba Ligi kuu TPL leo 1 January 2019

Uongozi wa Juu wa Klabu ya Simba msomaji wa Kwataunit.co.ke kupitia kwa Mtendaji wake Mkuu Crescentus Magori umefunguka kuhusiana na kinachoendelea kati Ya Simba na Kaizer Chief ya afrika kusini.
Magori ameelezea kuwa ni kweli klabu hiyo ya Afrika Kusini ilifanya mazungumzo ya mdomo lakini mpaka sasa hawajaleta ofa yao katika utaratibu unaotakiwa wa barua lakini kama wataileta basi bodi ya Simba itakaa kujadili lakini pia kumshirikisha kocha katika maamuzi.
Ni kweli walionyesha kumhitaji lakini mpaka sasa hawajaleta barua rasmi ya kumhitaji zaidi ya kufanya mazungumzo ya Mdomo wakileta bodi itafanya maamuzi na kama kocha atamruhusu kuondoka na kama ataondoka mrithi wake atakuwa nani lakini mpaka sasa hatujapata barua rasmi.
Alisema Magori.

 Install App bora ya michezo

No comments:

Post a Comment