Monday, 31 December 2018

Simba wafunguka kwa mara ya kwanza ishu ya Bwalya kutua Simba

Simba wafunguka kwa mara ya kwanza ishu ya Bwalya kutua Simba
Wakati washabiki na wanachama wa Simba wakiwa wanasubiri kujua nini hatma ya habari wanayoisikia juu ya Simba kuwa katika mipango ya kuitaka saini ya Straika hatari wa Nkana Fc Walter Bwalya uongozi wa Simba umefunguka kila kitu kuhusu taarifa hizo.

Ratiba Ligi kuu TPL leo 1 January 2019

Mtendaji mkuu wa Simba Crescentus Magori ameweka wazi kuwa hakuna kinachoendelea kati yao na Walter Bwalya na hata kama kitakuwepo basi siyo kwaajili ya kimataifa kwani mchezaji hyo ameshacheza ligi hiyo hivyo sheria zinambana.
“Tutamsikiliza Mwalimu nimepanga kukutana naye kesho ameona wachezaji Tanzania ameona wachezaji nje ya Nchi, Hivi vitu vilitungwa tu sijawahi kumsikia mwalimu akimzungumia Walter Bwalya , Kwanza Walter Bwalya ameshacheza michuano ya Kimataifa hawezi tena kucheza kama atazungumziwa labda kwaajili ya msimu ujao na siyo sahivi.”

 Install App bora ya michezo

No comments:

Post a Comment