Monday, 31 December 2018

Kiasi ambacho Simba imepata baada ya kuingia Makundi

Kiasi ambacho Simba imepata baada ya kuingia Makundi
Simba kwa sasa wanafuraha ya kutosha mara baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya makundi klabu bingwa barani Afrika mara baada ya mara ya mwisho kufanya hivyo mwaka 2003 kipindi hiko ikiwa kundi moja na timu za Enyimba, Ismaily ya Misri na Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast.
Simba kwasasa wanafurahia mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya makundi na kama unakumbuka mara baada ya kufuzu hatua ya makundi kocha wa Simba Patrick Aussems alionekana kuwa mwenye furaha kubwa sana

Alichokisema Aussems kuhusu uwezo wa Zana Coulibaly

Furaha ya Aussems ilitokana na kufanikisha moja ya makubaliano ya kuhakikisha Simba inafika hatua ya Makundi.
FEDHA WANAZOPATA SIMBA KWA KUTINGA MAKUNDI.
Kwa Kufanikiwa tu Kuingia hatua ya Makundi basi klabu ya Simba na klabu nyingine zilizotinga hatua hiyo zimejihakikishia kiasi cha dola 550,000.
Kiasi hiki msomaji wa Kwataunit.co.ke ni zaidi ya Shilingi za kitanzania Bilioni 1.2 na kiwango kitakuwa kikiongezeka kadiri timu inavyozidi kwenda hatua za mbele kama robo fainali, Nusu Fainali na Fainali.

No comments:

Post a Comment