Wasanii watakaofanya onesho Jumatato hii katika Tamasha la Wasafi
Festival nchini Kenya kutoka Tanzania wamepokewa kwa shangwe kubwa na
Wakenya hapo jana. Awali
show hiyo iliingiwa na sitofahamu baada ya msanii Diamond na Rayvanny
kutoruhusiwa kufanya onesho nje ya nchi baada ya kufungiwa na BASATA kwa
kosa la kuimba wimbo Mwanza ambao ulifungiwa na baraza hilo. Lakini
mapema jana baraza hilo lilitoa ruhusa kwa waimbaji hao ya kufanya
enesho kwa madai adhabu ya kufungiwa ilikuja kwa wawili hao wakati
tayari wameshaingia makubaliano ya enesho la Kenya.
Baada ya team
hiyo kuwasili nchini Kenya, Rais wa WCB Diamond Platnumz aliwataka
mashabiki kukaa mkao wa kula kwaajili ya enesho hilo la aina yake.
“Earlier
Today in MOMBASA!!!…. Kesho kwa Pamoja Tunaandika Historia
ya #WasafiFestiVal208 kwa Mara ya Kwanza ndani ya Kenya Tena Mjini
MOMBASA!!!….. tafadhali nunu ticket yako sasa kupotia Mookh.com au wahi
Mapema Getini maana najua kabisa ticket ukichelewa zigakiwa shida….. na
usije kulalamika umekosa…. follow @nrgradioke kwa Taarifa zaidi!!!!,”
aliandika Diamond.
No comments:
Post a Comment