Mashabiki wa klabu ya Manchester United hii leo wanahamu kubwa ya
kumshuhudia kocha wao mpya, Ole Gunner Solskjaer akishuka kwenye uwanja
wa nyumbani wa Old Trafford kwa mara ya kwanza toka kukabiziwa timu hiyo
ambapo atawakabili Huddersfield. Mashetani
hao wekundu wakiwa chini ya Solskjaer walipata ushindi wa jumla ya
mabao 5 – 1 dhidi ya Cardiff City kwenye mchezo wake wa kwanza siku ya
Jumamosi iliyopita. Hiyo
ilikuwa ni mara ya kwanza kwa United kufunga mabao mengi kwenye mchezo
mmoja tangu mara ya mwisho ilipowahi kufanya hivyo chini ya kocha Sir
Alex Ferguson ambapo walitoka sare ya 5-5 dhidi ya West Brom mwezi Mei
mwaka 2013. Kwenye
mchezo wao huko Wales, mashabiki wa United walitoa heshima zao kwa
Solskjaer kupitia mabango yaliyoandikwa ’20LEGEND’ ambapo siyo aina mpya
ya mabango bali yaliwahi kutumika kipindi hicho wakati kocha huyo akiwa
mchezaji akivalia jezi namba 20 kabla ya kustaafu.
No comments:
Post a Comment