Thursday, 27 December 2018

Post ya Mo Dewji baada ya Simba kutolewa na Mashujaa

Post ya Mo Dewji baada ya Simba kutolewa na Mashujaa
Jana ilikuwa ni moja ya Siku ambayo ni kama ilijirudia kwa msimu uliopita kwa Simba kutolewa mapema zaidi katika michuano ya Azam Sports Federation Cup
Simba mwaka jana ilikubali kichapo kutoka kwa Green Warriors iliyokuwa ligi daraja la pili kipindi hiko lakini mwaka huu katika hali isiyotarajiwa Simba wamejikuta wameondolewa na timu ya daraja la chini tena ligi daraja lwa Kwanza Mashujaa kutoka Kigoma kwa bao 2 kwa 3.

Download ,Install App bora ya michezo

Mwaka Jana baada ya Simba kutolewa Kocha mcameron Joseph Omog alifukuzwa Simba baada ya Mo Dewji kuandika tweet ambayo ilikuwa ni ya Kumuomba Joseph Omog Kujiuzulu.
Tweet Ilisomeka Hivi
-Kwa kuwa bado sina mamlaka ya maamuzi kwenye klabu ya Simba, kama mwanachama na mshabiki wa Simba, namuomba Joseph Omog kwa heshima na taadhima ajiuzulu,”
Jana baada ya Simba kufanyiwa kitendo kama kilekile cha kutolewa mapema kombe la Shirikisho mambo yanaonekana kwenda tofauti kwa Mbelgiji Patrick Aussems kwani jambo lililofanyika kwa Omog yeye halijamkuta na Mo dewji aliandika ujumbe Huu hapo chini kuwa maisha ni lazima yasonge mbele bila Kufafanua.

Download ,Install App bora ya michezo

No comments:

Post a Comment