Sunday, 30 December 2018

Usichokijua kuhusu mabao mawili ya Makambo dhidi ya Mbeya City

 
Usichokijua kuhusu mabao mawili ya Makambo dhidi ya Mbeya City
Yanga jana iliendeleza rekodi yake ya Kucheza bila kupoteza mechi huku waliokuwa na rekodi kama ya Yanga timu ya Azam Fc ikijikuta ikichezea kichapo mbele ya wakata miwa kutoka Manungu Turiani Mtibwa Sugar.
Yanga jana iliwachakaza Mbeya City bao 2 kwa 1 ikicheza uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku mabao yote yakifungwa kupitia mguu wa Makambo na Kichwa chake ambacho kimekuwa kikiwapa shida sana mabeki wanapopanda naye hewani.

Wachezaji wanaoongoza kwa Magoli ligi kuu Tanzania bara TPL 2018/2019

USICHOKIJUA KUHUSU MAGOLI MAWILI YA HERITIER MAKAMBO
Heritier Makambo licha ya kuwa na magoli 11 kibindoni huku akiwa ndiye kinara kwa sasa baada ya kuwazidi mbio wenzake Said Dilunga wa Ruvu Shooting na Eliud Ambokile lakini kuna namna magoli hayo ya Makambo yamekuwa na maana sana kwake.
Toka Makambo ameanza kufunga magoli ligi kuu TPL msomaji wa Kwataunit.co.ke hakuwahi kufunga mabao mawili katika mchezo mmoja na mchezo dhidi ya Mbeya City ndiyo imekuwa mechi yake ya Kwanza kufunga bao mbili katika mechi moja.
Makambo alifunga bao 1 katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar,Coastal Union, Alliance, Lipuli , Mwadui Fc, Kagera Sugar, JKT, Biashara United, Ruvu Shooting
Mechi hizo tisa hapo juu alizofunga alikuwa akifunga goli moja pekee lakini katika mechi dhidi ya Mbeya City akifanikiwa kutupia bao 2 kwa mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment