Mchezaji wa klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel
Messi ambaye pia ndio kapteni wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina
amefanikiwa kuvunja rekodi ya wachezaji mbalimbali barani Ulaya.

Messi akiwa Barcelona amefanikiwa kucheza michezo 435, rekodi ambayo amempita mchezaji kutoka Nchi Ujerumani Gerd Müller
aliyeitumikia Bayern Munich ambaye alifikisha magoli 365 akifuatiwa na Mreno anayeitumikia Juventus lakini magoli haya aliyapachika akiwa La liga Cristiano Ronaldo ambaye alifunga magoli 311.

Katika
ligi kuu nchini Uingereza anayeongoza kufunga magoli mengi ni Alan
Shearer mwenye magoli 260, Ligi kuu nchini Ufaransa Ligue 1 anayeongoza
ni André-Pierre Gignac ambaye alikuwa na magoli 103, Ligi kuu nchini
Italia Seria A anayeongoza ni Silvio Piola, mwenye magoli 274 na ligi
kuu nchi Ujerumani ni Gerd Müller mwenye magoli 365 na La liga ndio
Messi mwenye magoli 400.
Download ,Install App bora ya Habari na michezo
Messi ambaye anaitumikia Barcelona msimu wa 14 hadi hivi sasa amefanikiwa kuvunja rekodi ya kufikisha magoli 400 katika ligi 5 bora barani ulaya ambazo ni Ligi kuu nchini Uingereza PL, Ligi kuu nchini Ufaransa Ligue 1, Ligi kuu nchini Ujerumani, Bundasliga, Ligi kuu nchini Italia Seria A na Ligi kuu nchini Uhispania Laliga kwa kufikisha magoli hayo 400.
aliyeitumikia Bayern Munich ambaye alifikisha magoli 365 akifuatiwa na Mreno anayeitumikia Juventus lakini magoli haya aliyapachika akiwa La liga Cristiano Ronaldo ambaye alifunga magoli 311.
No comments:
Post a Comment