Friday, 18 January 2019

Ratiba ligi Kuu Tanzania TPL Leo 19 January 2019

Ratiba ligi Kuu Tanzania TPL Leo 19 January 2019
Ligi kuu soka ya Tanzania bara itaendelea leo 19 January 2019 katika viwanja mbali mbali Tanzania.
Mechi ya mapema itakuwa kati ya Coastal Union dhidi ya African Lyon ambayo Itaanza saa nane Mchana.
Mechi nyingine itakuwa kati ya Mtibwa Sugar watakaokuwa wenyeji uwanja wa Manungu kuwakaribisha vijana kutoka Iringa Lipuli Fc.
Nao Singida United watakuwa nyumbani Namfua Stadium kuwakaribisha vijana wa Mjini Dar Es Salaam katika manisapaa ya Kinondoni KMC ambao gari limewaka kwa sasa.
Yanga wao watakuwa ugenini kucheza na Chama la wana Stand United katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Nao Azam Fc watakuwa nyumbani uwanja wa Azam Complex Chamazi kuwakaribisha vijana wa Mwadui Fc kutoka wilayani kISHAPU mkoani Shinyanga.

Download ,Install App bora ya michezo

No comments:

Post a Comment