Salamba : Sijashuka Kiwango
MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, Adam Salamba, amesema kiwango chake hakijashuka hivyo si kila siku anaweza kuwa fiti kama mashabiki wanavyotaka.
Alitoa kauli hiyo baada ya mashabiki kudai hajaitendea haki nafasi yake katika baadhi ya mechi alizocheza kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi yaliyomalizika juzi visiwani Zanzibar, huku Azam ikitwaa ubingwa.
Akizungumza nasi, Salamba alisema anapambana kila siku kuipigania timu yake, lakini pia siku hazifanani hivyo mchezaji hawezi kuonekana bora kila wakati.
“Kuna wakati mchezaji anaweza kuonyesha kiwango bora na kumvutia kila mmoja, lakini siku nyingine akashindwa kufanya vizuri na hali hii inawakuta wengi.”
Hata hivyo, aliongeza kuwa licha ya kuukosa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, lakini anaamini bado wanayo nafasi ya kutwaa ubingwa katika mashindano mengine.
Akielezea kuhusu mipango ya kwenda kucheza soka la kulipwa, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu tayari limefika kwa uongozi na meneja wake pia analishughulikia.

No comments:
Post a Comment