Tuesday, 1 January 2019

Ujumbe wa Haji Manara akimtaka baba yake aachane na Yanga

Ujumbe wa Haji Manara akimtaka baba yake aachane na Yanga
Baba yake na Afisa habari wa Simba Haji Manara, Mzee Sunday Manara “Computer ” ni moja ya wachezaji waliocheza Yanga kwa mafanikio makubwa sana.
Sasa juzi wachezaji wa zamani wa Yanga walikutana na Kocha wa Yanga Zahera Mwinyi kuzungumza naye mambo mbalimbali kuhusu Klabu yao na moja ya wachezaji waliohudhuria alikuwepo Sunday MANARA.
Baada ya kikao cha wachezaji hao na kocha muwakilishi wa wachezaji wa zamani Sunday MANARA aliongea na waandishi wa habari kuelelezea walichokuwa wakizungumza na kocha
Lakini leo mwanaye Haji Manara amepost kipande kifupi cha baba yake akizungumza kuhusu Yanga na kumuomba aachane na Yanga.
Ujumbe wake.
Daaah huyu ni baba yangu mzazi na nampenda sana ila hata sijui why alicheza hili team na nnajua hv sasa mijitu ya Yanga inajitahidi kumtumia ili kunififisha mm , lakini hawataweza, yy ni Gongowazi mm ni Simba
Duniani watu hurithi mali,hawarithi ushabiki wa team!!
Hahahahaha my dad this is my time achana na hyo mitimu ya ajabu ajabu
Hiyo team unayoshabikia ni ya watu wa zamani enzi za kina Unju bin Unuki, njoo Simba kuna Chama na kina Kagere, halaf yupo MO na mwanao, baba baba pls mm mwanao nisikilize..

No comments:

Post a Comment