Tuesday, 15 January 2019

Yusuph MANJI kama utani leo anarejea Yanga

Yusuph MANJI kama utani leo anarejea Yanga
WAKATI yanga ikiwa inashuka leo kuvaana na Mwadui Fc ya Mkoani Shinyanga katika uwanja wa taifa nakukumbusha tu leo inaweza ikawa ni habari njema kwa wana Yanga.

Download ,Install App bora ya Habari na michezo

Habari njema kivipi? Habari njema kwasababu leo 15 January 2019 ndiyo siku ambayo kulingana na barua iliyosomwa na Mwenyekiti wa wadhamini klabu ya Yanga George Mkuchika leo Yusuph Manji anarejea rasmi kama mwenyekiti wa Yanga kwa kuanza kufanya kazi za kiofisi ndani ya klabu ya Yanga.
Wanachama wengi wanasubiri kuona kama ni kweli Manji ataibuka makao makuu ya Yanga na kuanza kufanya kazi zake kama kawaida huku Taarifa za chini chini zikieleza kuwa huenda manji akaibuka uwanja wa Taifa kushuhudia mechi kati ya Yanga dhidi ya Mwadui Fc.

Download ,Install App bora ya Habari na michezo

No comments:

Post a Comment