Download ,Install App bora ya michezo
Zahera: Simba wasipofanya hivi 5 za Congo zitajirudia
Wakati Simba ikiwa inaondoka leo kuelekea nchini Misri kwaajili ya mchezo wa hatua ya Makundi klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Al Ahly 2 February 2019 kocha wa Yanga amewapa ushauri kocha na viongozi wa Simba kuelekea mchezo huo.
Zahera amefunguka kuwa Simba ni lazima wahakikishe wanawaweka sawa wachezaji kisaikolojia kwani wasipofanya hivyo zile goli tano za Congo Simba wakicheza dhidi ya As Vita zinaweza kujirudia.
Zahera Mwinyi msomaji wa Kwataunit.co.ke amekuwa muwazi zaidi kwenye mazungumzo yake ameeleza kuwa asilimia sitini ya maandalizi ni lazima wahakikishe wachezaji wanakaa sawa kisaikolojia na asilimia 40 mbinu za Kimchezo.
” Inaweza kujirudia kile kilichotokea Congo kama wachezaji hawatawekwa sawa kisaikolojia kwani kile kindonda cha tano bado wachezaji wanacho kwahiyo inapaswa wachezaji wapone kabla ya mechi ya Al Ahly. ”
Alisema Zahera.
No comments:
Post a Comment