Monday, 28 January 2019

Zahera ataja mchezaji mpya ambaye Fei na Tshishimbi lazima wajipange


Zahera ataja mchezaji mpya ambaye Fei na Tshishimbi lazima wajipange
Kocha Maarufu zaidi pengine kuliko wote msimu huu wa Ligi kuu soka ya Tanzania Bara TPL Zahera mwinyi ameendelea kufunguka kuhusu mipango ya kikosi chake cha Yanga kuelekea mechi za Fa na za Ligi kuu soka ya Tanzania bara.
Zahera mwinyi amefunguka mengi ikiwemo ni kuelekea mchezo kati ya Yanga na Simba huku kocha huyo akisema kuelekea mchezo huo atakuwa na kikosi imara zaidi kuliko kile cha mzunguko wa Kwanza.
Kocha huyo pia akiongelea suala la nafasi ya vijana kwenye kikosi cha wakubwa amesema amekuwa akitumia wachezaji wengi vijana kama Kabwili, Maka Edward, Paul Godfrey na wengineo huku akimsifia kinda mwingine kuwa ni lazima Papy Tshishimbi na Feisal Salum wajipange.
Mchezaji huyo msomaji wa Kwataunit.co.ke ni Gustavo Simon kinda kutoka U20 aliyeonyesha cheche za kutosha katika michuano ya Mapinduzi Cup,
Zahera alisema mchezaji huyo ni moto sana na ni lazima viungo waliopo wajipange kutokana na uwezo wa mchezaji huyo ambaye huenda akaanza kuonekana raundi ya pili akiwa na kikosi cha Yanga

No comments:

Post a Comment