Mara nyingi tunapofikiria namna ya kumpata mwenza sahihi,
huwa tunaangalia ishu ya kumpata yule mwenye mapenzi ya dhati lakini
kumjua anayekupenda kwa dhati, anayeweza kukupatia kile ulichokitarajia
ni vigumu sana.
Ndiyo maana hapa chini nimekupa vigezo saba vya mtu ambaye anakupenda kwa dhati na anafaa kuwa mwenza wako endapo mtakuwa tayari mmeshaanzisha uhusiano wa kawaida.
Mguso wa hisia: – Hakika mapenzi ni mguso wa hisia, kwa maana hiyo kigezo kikuu cha kuzingatia kwa mtu anayestahili kuwa mwenzi wako wa ndoa ni vile ambavyo hisia zake umeziteka. Hali kadhalika na wewe mwenyewe ulivyotekwa naye.
Amani na furaha vikitawala kati yenu unajiona upo huru kwa kila kitu na mnapokuwa hamuelewani kila kitu kwenye akili yako unaona hakiendi. Vivyo hivyo na yeye kwamba amani ipo pale mnaelewana na inatoweka mnapokosana. Huyo ni wazi mnaendana.
Kutosheka: – Ukiwa naye unajisikiaje? Umetosheka eeh? Akiwa mbali inakuaje, unahisi kuna upungufu mkubwa? Vipi na yeye anajiona hivyohivyo? Kama jibu ni ndiyo maana yake mnaendana kwa sababu ukamili wako unamtegemea yeye, hali kadhalika na yeye.
Anakata kiu yako yote? Na upande wake inakuaje? Ikiwa ni hivyo, basi anatosha kuwa mwenzi wako wa maisha.
Malengo: – Kila mtu anapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi, lengo lake huwa ni kudumu. Achana na hulka za viruka njia. Pointi hii inakujenga kujua matarajio ya mwenzako kuhusu wewe. Anakuhitaji kwa maisha yake yote au yupo na wewe kwa sababu hana pa kwenda?
Wengi wapo kwenye majuto kwa sababu waliingia kwenye ndoa na watu ambao hawakuwa na nia ya dhati nao, bali walijichanganya baada ya kukosa uelekeo.
Suala la mawasiliano: – Anapenda kuwasiliana na wewe, ukimtumia SMS anaijibu ‘fasta’. Hatengenezi sababu ya kutowasiliana na wewe, daima anaona njia pekee ya kuwaweka karibu hata kama mpo mbali ni kuwasiliana. Nawe unampigia simu kwa wakati, unasikia raha kupokea ujumbe wake naye anaona fahari kupigiwa simu na wewe.
Kama hali hiyo ipo, basi upendo wa kweli upo na hiyo inatosha kuthibitisha kwamba mnaendana. Ukituma SMS naye akachelewa kujibu ni wazi haoni umuhimu wako.

No comments:
Post a Comment