Milipuko na milio ya risasi yasikika katika eneo la 14 Riverside,
Nairobi kunakopatikana hoteli ya DusitD2. Milipuko miwili mikubwa ya
risasi ilisikika na baadaye ufyatuaji wa risasi.
Watu kadha wamejeruhiwa na wanahudumiwa na maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu wakisaidia na watu wengine wa kujitolea. Mmoja wa majeruhi amesafirishwa kupelekwa hospitalini. Maafisa wa polisi wamefika eneo hilo, katika jumba hilo ambalo lina hoteli yakifahari na afisi za kampuni mbalimbali. Baadhi
ya watu waliokwama kwenye vyumba vya jumba hilo wamekuwa wakiandika
ujumbe kwenye mitandao wa kijamii wakieleza kwamba wamekwama, au
kujificha. Mkuu
wa polisi wa uchunguzi wa jinai Bw George Kinoti ni miongoni mwa
maafisa wakuu wa polisi waliofika kuratibu operesheni ya kuokoa watu
waliokwama ndani. Magari kadha yanawaka moto katika maegesho ya jumba hilo.
No comments:
Post a Comment