Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (Metl) imepata pigo
baada ya kufutiwa umiliki wa mashaba sita na Serkali yenye ukubwa ekari
12,915.126 yaliyopo Korogwe jijini Tanga.
Uamuzi
huo wa kufutiwa umiliki huo ulitangazwa jana na Naibu Waziri wa ardhi
nyumba na maendeleo ya makazi Angeline Mabula mara baada ya kumaliza
kutembelea mashamba hayo ya METL, kampuni ambyo inongozwa na
mfanyabiashara mkubwa hapa nchini Mohammed Dewij, alimaarufu Mo Dewij.
Mashamba
yaliyofutiwa kibali yako sita kati ya 14 yanayomilikiwa na kampuni hiyo
na yaliyopo katika eneo la Mombo, Mabango pamoja na Kwalukonge huko
wilayani Korogwe mkoani Tanga.
Naibu waziri huyo alisema uamuzi
huo umekuja baada ya ushauri uliotolewa na Halimashauri ya Wilaya ya
Korogwe kutokana na kutoendelezwa kwa muda sasa na ili kuleta nidhamu
kwa watu waliokabidhiwa rasilimali za Serikali kuzingatia masharti ya
uwekezaji.
.
Mabula
aliongeza mapendekezo hayo yaliwasilishwa kwa Rais Magufuli na Wizara
ya ardhi ikafanya ufuatiliaji katikaHalimashauri husika, alisema baada
ya kujiridhisha walirudisha mapendekezo wa Rais na kuridhia.
Aliongeza
uamuzi huo wa Rais kuridhia unabatilisha mashaba 6 kati ya 14
yanayomilikiwa na Mohammed Enterprises na unalenga kuhakikisha kuwa wote
walipewa maeneo kwa ajili ya uwekezaji wanazingatia masharti ya
uwekezaji na taratibu za uwekezaji. Naibu
Waziri aliongeza kuwa mashamba yaliyobakia ambayo hayajafutiwa kibali
yanawekewa utaratibu kwa nia ya kuboreshwa kwa kuwa baadhi yake
yanahitaji maboresho ili yafanye kazi.
Na kuitaka Halimashauri ya
wilaya ya Korogwe kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi katika eneo
la mashamba yaliyofutwa na watakaopewa eneo katika mashamba hayo ni
wananchi waliokuwa wakiishi katika mshamba hayo na sehemu iliyobaki
atafutwa mwekezaji mwingine kwa kuwa lengo la Serikali ni kuwa na
wawekezaji wa viwanda. Mabula
alimpongeza mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigella kwa kufanya kazi
nzuri ya kufuatilia na kusimamia maagizo mbali mbali tangu Mh. Rais
alipoanza kubatilisha mashamba ambayo hayajaendelezwa katika mkoa wake.
Baada
ya hapo mkuu huyo wa mkoa aliongea na kuwataka wananchi wa Korogwe
kutovamia maeneo ya mashamba yaliyobatilishwa hadi hapo Halimashauri ya
wilaya ya Korogwe itakapopanga matumizi bora ya ardhi katika mashamba
hayo.
Alisema
ndani ya wiki hii ataitisha mkutano na wataalamu wa sekta ya ardhi
katika mkoa huo pamoja na wale wa bodi ya mkonge kuangalia matumizi ya
ardhi iliyobatilishwa kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment