Mesut Ozil ameanza kuonekana kusababisha matatizo ndani ya klabu ya AC
Milan baada ya Paolo Maldini ambaye ni Mkurugenzi wa maendeleo ya
michezo na mikakati dhidi ya Mkurugenzi Mtendaji wa timu hiyo, Ivan
Gazidis.
Kiungo huyo wa Ujerumani amekuwa siyo chaguo la kocha, Unai Emery hivyo yupo mbioni kuondoka Emirates.
Ozil amekosa kuanzishwa kwenye michezo minne iliyopita licha ya kuwa anatoka kuuguza majeraha.
Kwa mujibu wa gazeti la michezo kutoka Italia, Carriere dello Sport limeeleza kuwa mahusiano baina yaGazidis na Maldini yamekuwa siyo ya kuridhisha juu maamuzi ya kumsajili Ozil. Gazidis
ambaye amewahi kuihudumia Arsenal kama Mkurugenzi kwa miaka 10 na
kufanikiwa kupata nafasi hiyo ndani ya miamba ya soka ya AC Milan mwaka
2017 amekuwa akipinga kusajiliwa kwa Ozil.
Akiamini kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 30, hatoweza kufiti kwenye timu hiyo kutokana na umri wake kuwa umeenda sana.
Legendari
wa klabu hiyo ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo na
mikakati yeye anahitaji nyota huyo Ozil kusajiliwa.
Ozil ambaye analipwa pauni 350,000 kwa wiki kwa muda mrefu amekuwa siyo chaguo la kwanza ndani ya timu.
No comments:
Post a Comment