Wednesday, 2 January 2019

Wapinzani wa Simba CAF wapata Pigo

Wapinzani wa Simba CAF wapata Pigo
HABARI njema kwa Simba ni kwamba wapinzani wao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, AS Vita ya DRC Congo, wamepata pigo baada ya winga wake matata Mukoko Batezadio, kutimkia IR Tangier ya Morocco.
Mukoko amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Morocco wenye thamani ya dau la dola 400,00 sawa na takribani shiling milioni 850 za Kitanzania.
Kuondoka kwa winga huyo kunaweza kuwa nafuu kwa Simba kwani alikuwa moja ya wachezaji tegemeo wa klabu hiyo kutokana nakasi aliyonayo.
Simba imetinga hatua ya makundi ikipangwa kundi D sambamba na Al Alhly ya Misri, JS Soura ya nchini Algeria pamoja na ASVita ya Congo.
Simba wataanza kampeni yao hiyo ya makundi wakikabiliana na Soura Januari 12 Uwanja wa Taifa na Januari 18 watasafiri kwenda Congo kuwakabili AS Vita iliyopata pigo hilo.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara walianza safari yao hiyo ya kutinga hatua ya makundi wakiwafunga Mbabane Swallosya Eswatini jumla ya mabao 8-1 wakianza kuwafunga mabao 4-1 Uwanja wa Taifa nabaadaye kuachia kipigo cha mabao 4-0 ugenini.
Hatua iliyofuata walikutana na Nkana FC ya Zambia na kuwafunga jumla ya mabao 4-3, wakianza kufungwa mabao 2-1 ugenini kabla ya kushinda mabao 3-1 Uwanja wa Taifa.
Dimba

No comments:

Post a Comment