Zlatan amchana Ronaldo baada ya kusema anafuata changamoto mpya Juventus “Changamoto ni kwenda timu ya daraja la kwanza na kuisaidia kuwa bingwa sio Juventus”
Baada ya Cristiano Ronaldo kuhama Real Madrid na kwenda timu ya
Juventus ya nchini Italia, alipohojiwa alinukuliwa akisema kuwa ameamua
kujiunga na timu hiyo ikiwa ni sehemu ya kubadilisha maisha na kutafuta
changamoto mpya katika maisha ya kazi yake ya soka ambayo amekuwa
akiifanya kwa muda mrefu. Ronaldo
alifika mbali zaidi na kuamua kumshawishi kwa kutoa kauli hadharani
mpinzani wake Lionel Messi nae kujaribu kuhama timu ili kutafuta
changamoto mpya katika kazi yake ya soka, kwani Lionel Messi amekuwa
akicheza timu moja tu FC Barcelona kwa miaka yote ukilinganisha na
Ronaldo aliyewahi kucheza Ligi ya kwao Ureno, England, Hispania na sasa
Italia. Sasa
mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic
ameikosoa kauli ya Ronaldo kuita Juventus ndio sehemu aliyokwenda kupata
changamoto mpya huku ikidaiwa kuwa katoa kauli kuwa Messi hana haja ya
kuhama Ligi ndio adhihirishe ubora wake, Ronaldo kama angetaka
changamoto mpya basi angeenda timu ya madaraja ya chini na kuhakikisha
inapanda Ligi Kuu na kutwaa Ubingwa. .
“Cristiano
Ronaldo anazungumzia kuhusiana na changamoto mpya? Anaita ni changamoto
mpya Kwenda klabu ambayo tayari ni kawaida kushinda Serie A? kwa nini
asingeamua miaka michache iliyopita kwenda katika timu ya daraja la pili
na kuisaidia kupanda Ligi Kuu na hatimaye kupanda na kutwaa Ubingwa?
Kujaribu kuwa Bingwa na timu ya daraja la pili na kuipeleka juu hiyo
ndio anaweza kuita changamoto” alisema Zlatan Ibrahimovic Kwa
upande wa Ronaldo kwa sasa akiwa na Juventus ambayo ndio msimu wake wa
kwanza ndio anaongoza katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu ya nchini
Italia akiwa tayari amepasia nyavu mara 14 akifuatiwa na Krzysztof
Piatek anayecheza timu ya Genoa akiwa amepasia nyavu mara 13.
No comments:
Post a Comment