Pande zote mbili za kisiasa nchini Marekani bado zinavutana kuhusu
ujenzi wa ukuta anaotaka kujenga Rais Donald kwenye mpaka na Mexico
hazijapata ufumbuzi jinsi fedha zitakavyotumiwa katika kuujenga ukuta
huo.
kwa
mujibu wa DW Swahili, Katika taarifa ya pamoja, viongozi wa chama cha
Demokratik seneta Chuck Schumer na mwenzake, spika Nancy Pelosi,
wamemlaumu rais Donald Trump kwa mkwamo huo katika shughuli za serikali
na pia kwa kuitumbukiza nchi kwenye matatizo. Wamesema Trump alitaka
shughuli za serikali zikwame lakini kwa sasa anaonekana hajui vipi
atajiondoa kwenye sakata hilo.
Kwa upande wake Trump alijisifu
kwamba angeweza kuzikwamisha shughuli za serikali kwa ajili ya kupigania
ujenzi wa ukuta, lakini sasa anawalaumu wanachama wa Demokratik kwa
kukataa kuiunga mkono kura iliyohitajika kupitisha muswada wa bunge juu
ya kuridhia dola bilioni 5.7 anazotaka kwa ajili ya kujengea ukuta huo.
Viongozi hao wa chama cha Demokratik wameelezea hasara kubwa iliyotokea
kwenye soko la hisa la Wall Street pamoja na uharibifu uliosababishwa na
hatua ya Trump ya kumuachisha kazi waziri wake wa ulinzi.
Ni
mpaka hapo Trump, ambaye anataka kuujenga ukuta huo baina ya Marekani
na Mexico, na wanachama wa chama cha Demokratik, ambao wanaipinga hatua
yake hiyo watakapokubaliana, sehemu ya shughuli za serikali ya Marekani
zitaendelea kufungwa.
Jana tarehe 25 mwezi wa 12 ilikuwa siku ya
Krismasi na mkwamo huo umeingia katika siku yake ya nne na wala hakuna
dalili kuwa hali hiyo itafikia mwisho wake hivi karibuni.
Viongozi wa chama cha Democrats. Kushoto: Chuk Schumer. Kulia: spika Nancy Pelosi
Wabunge
wengi wameondoka kutoka kwenye jiji la Washington kwenda kujiunga na
familia zao wakati ambapo kusherehekea Krismasi, rais Trump amebakia
katika ikulu baada ya kuahirisha mipango ya sherehe za Krismasi katika
makazi yake ya Florida.
Trump aliwaambia waandishi wa habari
katika ikulu siku ya Jumatatu aliposhiriki kwenye mahojiano ya simu
ambao ni utamaduni unaofanyika kila mwaka unaowashirikisha watoto na
safari hii sana walitaka kujua ni lini baba Krismasi atawafikia waliko?.
Trump amesema hakuna chochote kipya isipokuwa anachojua ni kwamba
Marekani inahitaji usalama katika mpaka wake.
Trump
alikutana Jumatatu na waziri wake wa ulinzi Kirstjen Nielsen na
viongozi wengine wa idara ya usalama huku mazungumzo yakiendelea nyuma
ya pazia kati ya wawakilishi wa serikali pamoja na wa vyama vya
Republican na Demokratik.
No comments:
Post a Comment